Kuna
muuzaji fulani hapa chuoni, anayeshughulika na bidhaa kama mahamri, chapati,
samosa, chips, smokies, na kadhalika.
Kwa mda mrefu nimekuwa nikimchunguza mienendo yake na nikagundua kwamba anatumia ujanja sana na kuwafyonza wanafunzi wenzangu.
Unaponunua kitu kama chips hivi, atafanya awezalo mpaka akunyanyase tu kwa ule uchache wa bidhaa hizo atakazokutilia. Utaondoka ukiwa sura umeivimbisha lakini utafanyaje na tayari kalameni keshatia ngwenje kibindoni? Wakati mwengine usipokuwa makini atakurudishia baki isiyo kamili ama hata ajifanye kasahau kabisa!
Tabia hii imekuwa ikinikera kwa mda mrefu lakini nikaweka tumaini kwamba, "Hata sungura mjanja alishikwa wavu likabaki shavu, kwani huyu ni nani asipatikane kwa nyavu siku moja?"

![]() |
| Uzito wa kiamsha kinywa |
Leo imekuwa siku kubwa sana kwangu. Nimeamka asubuhi na kama ilivyo ada,
nikatayarisha chai vizuri- tena ya mkandaa, na tangawizi ndani yake. Kisha
nikajitembeza hadi kwenye duka la vitafunio kwa lengo la kujipatia angalau
mahamri mawili ili niongeze uzito wa kiamsha kinywa eti.
Kufika pale nikakuta watu watatu wakihudumiwa na jamaa huyo huyo. Nikachomoa noti ya shilingi hamsini na kumwambia, "Unisaidie na mahamri mawili." Muuzaji huyo, kwa upole na uhakika, akachukua mfuko mweusi wa nailoni na kuanza kutumbukiza mahamri sasa. Basi nimehesabu mpaka yakafika sita! Wala sikusema jambo. Akanipa, nikayapokea kwa mikono miwili nikaanza kusubiri baki yangu ya shilingi ishirini- Hamri moja ni shilingi tano amba?
Kwa mshangao mkubwa na tabasamu ya ndani kwa ndani, sikuamini macho yangu nilipopokea kitita cha shilingi mia nne na sabini!

Bila kusita, nimezichukua kwa uzuri na kuondoka mara hiyo.
Nikatembea aste aste, kwa maringo na madoido mpaka chumbani kwangu ambako
nimejifanyia sherehe ya kibinafsi huku nikishukuru kwa bahati niliyoiangukia
siku ya leo. Kiamsha kinyua kimekuwa cha uzito si haba na mpaka sasa bado
nimefurahi. Tangu lini shilingi hamsini ikawa mia tanooo?
Ukweli mchungu ni kwamba sijamuibia - Kwani makini yake imepotelea wapi leo?

No comments:
Post a Comment