More about me...

My photo
Kilifi, Coast, Kenya
Informing is not only my profession but also passion

Welcome

Welcome

Wednesday, 4 July 2012

Airtel sparks a smile



Airtel, one of the leading telecommunication network providers in Kenya has finally done its thing.
Today, through its Limited Edition Klub254 Gear, it has made my day. My participation in this particular promotion was not in vain - I have won some amazing prizes! An airtel branded T-shirt, water bottle and 500/= credit.

Awarding me the prizes at the Eldoret Airtel Office, Mr. Donald said, "With this airtime, you can continue browsing and you could win more with Airtel Club 254..."
It was a nice experience and I promised to continue using Airtel network.
Club 254 enables you to choose 10 Airtel numbers, add them as friends and call them at only 1 bob per minute, apart from send them free sms all day! You can also access free Facebook through 0.facebook.com and free twitter through m.twitter.com. To join club 254, dial *254# and proceed- at only 1 bob per day.
To participate in the Limited Edition Klub254 Gear, just like this Airtel Facebook page.

Ujanja wa mwuzaji - Hasara kwa mwuzaji


Kuna muuzaji fulani hapa chuoni, anayeshughulika na bidhaa kama mahamri, chapati, samosa, chips, smokies, na kadhalika.
Kwa mda mrefu nimekuwa nikimchunguza mienendo yake na nikagundua kwamba anatumia ujanja sana na kuwafyonza wanafunzi wenzangu.
Unaponunua kitu kama chips hivi, atafanya awezalo mpaka akunyanyase tu kwa ule uchache wa bidhaa hizo atakazokutilia. Utaondoka ukiwa sura umeivimbisha lakini utafanyaje na tayari kalameni keshatia ngwenje kibindoni? Wakati mwengine usipokuwa makini atakurudishia baki isiyo kamili ama hata ajifanye kasahau kabisa!
Tabia hii imekuwa ikinikera kwa mda mrefu lakini nikaweka tumaini kwamba, "Hata sungura mjanja alishikwa wavu likabaki shavu, kwani huyu ni nani asipatikane kwa nyavu siku moja?"
Uzito wa kiamsha kinywa
Leo imekuwa siku kubwa sana kwangu. Nimeamka asubuhi na kama ilivyo ada, nikatayarisha chai vizuri- tena ya mkandaa, na tangawizi ndani yake. Kisha nikajitembeza hadi kwenye duka la vitafunio kwa lengo la kujipatia angalau mahamri mawili ili niongeze uzito wa kiamsha kinywa eti.
Kufika pale nikakuta watu watatu wakihudumiwa na jamaa huyo huyo. Nikachomoa noti ya shilingi hamsini na kumwambia, "Unisaidie na mahamri mawili." Muuzaji huyo, kwa upole na uhakika, akachukua mfuko mweusi wa nailoni na kuanza kutumbukiza mahamri sasa. Basi nimehesabu mpaka yakafika sita! Wala sikusema jambo. Akanipa, nikayapokea kwa mikono miwili nikaanza kusubiri baki yangu ya shilingi ishirini- Hamri moja ni shilingi tano amba?
Kwa mshangao mkubwa na tabasamu ya ndani kwa ndani, sikuamini macho yangu nilipopokea kitita cha shilingi mia nne na sabini!
Bila kusita, nimezichukua kwa uzuri na kuondoka mara hiyo.
Nikatembea aste aste, kwa maringo na madoido mpaka chumbani kwangu ambako nimejifanyia sherehe ya kibinafsi huku nikishukuru kwa bahati niliyoiangukia siku ya leo. Kiamsha kinyua kimekuwa cha uzito si haba na mpaka sasa bado nimefurahi. Tangu lini shilingi hamsini ikawa mia tanooo?
Ukweli mchungu ni kwamba sijamuibia - Kwani makini yake imepotelea wapi leo?